Background

Mei 25 – Siku ya Ukombozi wa Afrika ni uhamasishaji mkubwa zaidi wa kila mwaka wa Waafrika Wanaoinuka, kuvutia maelfu ya washiriki na kuunda mshikamano wa kimataifa juu ya mada fulani.
Image

Kuhusu Uhamasishaji wa Mei 25 - Historia

Siku ya Ukombozi wa Kiafrika ni maadhimisho ya kila mwaka ya uanzishaji wa Shirika la Umoja wa Kiafrika mnamo Mei 25, 1963. Pia ni maadhimisho ya uzinduzi wa vuguvugu la Africans Rising mnamo Mei 25, 2017. Katika siku za nyuma, vuguvugu la Africans Rising ilitumia Mei 25- Siku ya Ukombozi wa Kiafrika kutambua masuala ya mtiririko haramu wa fedha, utumwa, na afya. Sasa, kutokana na hali ya janga la Virusi vya Korona, uhamasishaji huu ni wakati muhimu wa kutoa wito kwa serikali, taasisi na biashara kuweka maisha mble ya maslahi yao ya kibinafsi na faida wakati wa mgogoro huu wa afya duniani.

Wiki ya Ukombozi wa Afrika 2022

Image

Bendera ya uhamasishaji wa mwaka wa 2022 inabadilika kutoka kutambulika kama Siku ya Ukombozi wa Afrika na itatambulika sasa, kama Wiki ya Ukombozi wa Afrika. Hii inaakisi jinsi tunavyohamasishana ambayo mara nyingi huchukua wiki nzima yenye shughuli badala ya siku moja tu na hivyo basi itasaidia kuondoa mkanganyiko katika akili za wanachama wetu. Vile vile inaonyesha vyema rekodi ya kihistoria. Mjadala kuhusu umuhimu wa umoja wa Afrika mnamo Mei 1963 haukuwa tukio la siku moja. Ilianza tarehe 23Mei1963 na ikakamilika kwa kutiwa saini Mkataba wa OAU, inayojulikana sasa kama AU, mnamo tarehe 25 Mei 1963.

Tarehe

Wiki ya Ukombozi wa Afrika itaadhimishwa kuanzia tarehe 23 Mei 2022 hadi tarehe 29 Mei 2022.

Mandhari na mada ndogondogo

Mwaka huu, uhamasishaji huu uko chini ya mada pana “Afrika, kwa Waafrika” ambayo inasisitiza hitaji la umoja na umiliki, katika kukabiliana na mapambano yanayowakumba Waafrika, yakiambatana na mada ndogondogo zinazopeana nafasi kuzingatia maeneo muhimu na mikondo ya uhamasishaji mnamo 2022. Tutaendesha kampeni pepe chini ya mada hii, pamoja na reli yetu #Rise4OurLives.

Mada pana:

Afrika, kwa Waafrika

``Waafrika`` inahusisha watu wote wenye asili ya Kiafrika popote walipo. Mada hii inaangazia tena wito wa kihistoria wa Marcus Garvey kwa Waafrika kuungana na kuchukua umiliki na udhibiti wa bara letu. Umuhimu wake katika nyakati za kisasa unaonekana hasa katika ule mwendo wa haraka wa mataifa makuu mamboleo pamoja na ya zamani, yakilenga rasilimali za Afrika.

Mandhari ndogo:

  1. Kuondoa ukoloni – kutimiza agenda ambayo haijakamilika ya kuumaliza ukoloni
  2. Haki ya kijinsia – kuhakikisha usawa wa kijinsia katika kuichonga Afrika Tunayoitaka
  3. Afya – ufikiaji sawa wa huduma bora za afya huku kukiwa na COVID-19
  4. Haki ya Hali ya Hewa na Mazingira – kuendeleza msukumo wa kufanikisha  haki ya hali ya hewa na mazingira kwa lengo la kuitimiza  #AfrikaTunayoitaka

Wito wa Kitendo:

Shughuli za kuashiria Ukombozi wa Afrika zitafanyika kuanzia tarehe 23 hadi 29 Mei 2022. Kujiandikisha Tukio la Wiki ya Ukombozi wa Afrika na sisi, jaza fomu hii fupi hapa: https://forms.gle/sYzg1kHdpMPPAXf6A 

jaza fomu hii fupi hapa:
No Content Available

Wasaidie Africans Rising wajenge Vuguvugu/Harakati imara ya haki, amani na heshima.

Tunaamini katika kuwaunganisha Waafrika kwa mabadiliko chanya, endelevu. Unapotoa mchango wako kwa Africans Rising, unatusaidia kuendelea na operesheni zetu na kuwafikia wanaharakati wa ngazi za chini wa Kiafrika kote barani na Ughaibuni/Diaspora .

This post is also available in: English Français العربية Português