Utambulisho Wetu

Utambulisho Wetu

Dira kuu ya Africans Rising imefafanuliwa katika Azimio la Kilimanjaro lililochapishwa wakati wa kuanzishwa kwake na kufanyiwa marekebisho na wanachama kwenye Kongamano Kuu la Mavuguvugu ya kiafrika

Azimio Letu

Vuguvugu linaazimia kwamba uharakati wa bara nzima la Afrika, mshikamano na ushirikiano wa kimalengo wa Waafrika utajenga mustakabali wanaotaka - haki, amani, hadhi na ustawi wa pamoja.

Dhamira Yetu

Kufanya kazi pamoja na, kujenga, kuimarisha, kuunga mkono, na kuinua mavuguvugu ya Waafrika mitaani, kitaifa au kikanda, mapambano ya mashinani na mavuguvugu ya kijamii kwa kuibua mashirika yanayoungwa mkono na mtandao unaowawezesha kuungana, kupata haki, amani, hadhi na ustawi wa pamoja wa kiafrika. Mtandao huu unawajibika kwa jamii wanazoziwakilisha na utakuwa na viwango vya juu zaidi vya maadili.

Historia ya Vuguvugu

Historia ya Africans Rising

Vuguvugu la Africans Rising lilitokana na mfululizo wa mashauriano na midahalo ya ana kwa ana na mitandaoni kati, na miongoni mwa mavuguvugu ya kijamii, mashirika yasiyo ya kiserikali, watu na makundi maarufu ya haki za kijamii, wasomi, wasanii, wanariadha, wanaharakati wa kitamaduni, mashirika ya kidini, vyama vya wafanyikazi na wengine, kote katika kanda zilizoidhinishwa na Umoja wa Afrika ikiwemo Ughaibuni. Vuguvugu la Africans Rising lilizinduliwa rasmi mwezi Mei 2017 ikizingatiwa kwamba mashirika ya kijamii ya Afrika yalihitaji kubuni mbinu mpya, shirikishi, na mwafaka za kufanya kazi ya mabadiliko ya kijamii.

Mkutano wa Uthibitishaji

Mkutano wa Uthibitishaji ulifanyika kati ya tarehe 23 na 24 Agosti 2016 katika Kituo cha Mafunzo cha MS cha Ushirikiano wa Maendeleo (TCDC), Arusha, Tanzania. Wajumbe 272 walihudhuria mkutano huo kutoka nchi 40 za Afrika pamoja na uwakilishi wa heshima kutoka Ughaibuni. Asilimia 51 ya wajumbe walikuwa wanawake na 60% walikuwa chini ya umri wa miaka 35. Mkutano huo kwa makusudi uliwaweka washiriki wake wote katika kiwango sawa na Dola za Marekani 397 zilichangwa kwa hiari katika harakati hizo.

Uzinduzi wa Africans Rising nchini Tanzania

Tangu kuanzishwa kwetu mwezi Mei 2017

Tangu kuanzishwa kwetu Mei 2017, tumeendelea kukuza ufahamu wa kina wa haja ya kurekebisha vuguvugu letu dhidi ya kanuni za usimamizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Mashauriano yetu yamefichua wasiwasi mkubwa kuhusu miundo ya jadi ya kisiasa, ushawishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na hata kwa mashirika ya kijamii. Vijana wa Afrika wana azma kubwa ya kujitenga na aina yoyote ya utambulisho na ni jukumu letu kuelewa upanafrika una maana gani kwa kizazi cha milenia. Uongozi wa kisiasa ambao haufanyi kazi kwa utaratibu umewafanya vijana wetu kudharau mustakabali wowote wa ushirikiano. Ndiyo maana kuna uthibitisho wa makubaliano kwamba Waafrika wanainuka lakini kwa masharti yao wenyewe na kwa sheria zisizo za kawaida.

Timu ya TCDC ikisherehekea 25May 2017