[vc_row][vc_column][vc_column_text]Vuguvugu la Africans Rising, linalolenga kufanikisha Haki, Amani na Utu lina furaha kutangaza kwamba wiki itakayoanzia tarehe 23 hadi 29Meiimetangazwa kuwa Wiki ya Ukombozi wa Afrika .. Uhamasishaji wa mwaka huu utaendeshwa chini ya mada “Afrika, kwa Waafrika”na unaonyesha hitaji mpya la umoja kati ya Waafrika kote ulimwenguni kumiliki, kudhibiti na kusimamia mambo yetu wenyewe.

Kila mwaka, Siku ya Ukombozi wa Afrika huadhimishwa tarehe Mei 25 kukuza umoja na mshikamano miongoni mwa watu pamoja na mataifa ya Afrika. Maadhimisho haya ni fursa ya kuhamasisha Waafrika wote – mashirika ya mashinani, vyama vya wafanyakazi, vikundi vya kijamii, mashirika ya wanawake, vikundi vya kidini, vikundi vya vijana, vyama vya mitaa, vyombo vya habari, watu binafsi – kuchukua hatua kwa mujibu wa mada au masuala maalum yenye umuhimu katika miktadha ya kimaeneo pamoja na ya kibarani. Africans Rising hutumia wiki nzima ya Mei 25 kuhakikisha kwamba Waafrika kote ulimwenguni wanaweza kushiriki katika ukumbusho huu, na vile vile kuchunguza mapana ya masuala yanayozikabili jumuiya za Kiafrika. Pamoja na mada yetu ya “Afrika, kwa Waafrika” mwaka huu, tunazitambua mada ndogo zifuatazo:

  • Kuondoa ukoloni – kutimiza agenda ambayo haijakamilika ya kuumaliza ukoloni
  • Haki ya kijinsia – kuhakikisha usawa wa kijinsia katika kuichonga Afrika Tunayoitaka
  • Afya – ufikiaji sawa wa huduma bora za afya huku kukiwa na COVID-19
  • Haki ya Hali ya Hewa na Mazingira – kuendeleza msukumo wa kufanikisha haki ya hali ya hewa na mazingira kwa lengo la kuitimiza #AfrikaTunayoitaka

[/vc_column_text][vcmp_space vcmp_height=”20″][vc_column_text]Historia ya Uhamasishaji ya Africans Rising kwa Ajili ya Siku ya Ukombozi wa Afrika

Mnamo tarehe 25, Mei, 2017, wafanyakazi wa kujitolea elfu mbili, washirika, wafuasi pamoja na marafiki walipanga jumla ya matukio na sherehe 300 katika nchi 42 za bara la Afrika na ughaibuni(Diaspora), kuashiria uzinduzi wa vuguvugu la Africans Rising. Mnamo tarehe 25 Mei 2018, uhamasishaji ulikuwa mkubwa zaidi kwani mamia ya hatua pamoja na matukio ya kibinafsi yaliandaliwa katika nchi 54 zikiwemo 6 zilizoandaliwa miongoni mwa jamii za Kiafrika za ughaibuni(diaspora). Mnamo mwaka wa 2019, shughuli zilihusisha, maonyesho ya filamu, ushirikiano na vyombo vya habari, kongamano la hadhara, mijadala ya jopo pamoja na shughuli zingine kadhaa kuhusu Utumwa Mamboleo. Mnamo 2020 na 2021, Africans Rising iliangazia afya na ustawi wa Waafrika na jamii za Kiafrika, kwa kuzingatia janga la COVID-19 pamoja na matokeo yake mabaya katika nyanja zote za maisha, kupitia kampeni yetu ya #Rise4OurLives. [/vc_column_text][vcmp_space vcmp_height=”20″][vc_column_text]Kuhusu Africans Rising

Vuguvugu la Africans Rising, linalolenga kufanikisha Haki, Amani na Utu ni vuguvugu la kijamii la Waafrika na watu wenye asili ya Kiafrika kote ulimwenguni linalofanya kazi ili kukuza mshikamano wa Afrika nzima na umoja wa madhumuni ya watu wa bara la Afrika.Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu katika africansrising.org na utufuate kwenye Twitter (@AfricansRising) , Facebook (AfricansRising), na Instagram (@Africans Rising).

Kwa habari zaidi wasiliana na: media@africans-rising.org
AU Ancel Langwa – Kiongozi wa Mawasiliano na Vyombo vya Habari, Africans Rising

Barua pepe: ancel@africans-rising.org | +237670011987[/vc_column_text][/vc_column][/vc_row]

Similar Posts